Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hii nayo kali! Mwamba akutwa na rundo la makopo ya mkojo chumbani

Mkojo 0000 Hii nayo kali! Mwamba akutwa na rundo la makopo ya mkojo chumbani

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyo ya kawaida kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Laiza, mkazi wa mtaa wa Kivukoni Kata ya Kalangalala Halmashauri ya Mji wa Geita, amekutwa na chupa nyingi zilizojaa mkojo chumbani kwake ambazo zinatoa harufu kali inayowaathiri majirani wa eneo hilo.

Akizungumzia tukio hilo mama mwenye nyumba hiyo pamoja na majirani zake wamesema wilikuwa wanasikia harufu mbaya kwa muda mrefu ikitokea katika chumba chake huku wakidhani pengine kuna mtu amefariki, kutokana na mwenye chumba kutoonekana muda mrefu.

Baada ya askari kujulishwa kwaajili ya upekuzi ndipo walipovunja mlango na kukuta hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live