Mjadala wa iwapo Harmonize anaghushi views kwenye mtandao wa YouTube upo mbali sana na kufikia kikomo kutokana na idadi ya views kazi za msanii huyo zinapata kwa sekunde za kuhesabu tu.
Ikumbukwe wiki jana, msanii huyo aligonga vichwa vya habari sana baada ya collabo yake na Ibraah kwa jina la Mdomo kugonga views zaidi ya milioni 1.3 chini ya sekunde 24 za kuhesabu tu.
Hili lilizua mjadala mkali baadhi wakisema dogo anazingua sana na kukubalika mno na mashabiki huku wengine wakisema ni robot aliweka inayobiringisha idadi ya views na si watu halisi wanaoingia pale na kutazama.
Mjadala huu ulionekana kutulia kidogo baada ya watu kama vile Mwijaku kujitokeza wazi na kuwapa changamoto wale wanaosema kwamba kama ni robot na wao waweke.
Lakini tena mjadala huu umeibuliwa upya na video ya msanii Diamond Platnumz, ya wimbo wa Wonder ambayo aliipakia Jumatatu na kinyume na ile ya Harmonize ambayo kwa sekunde 24 tayari views zilikuwa milioni 1.3, hii ya Diamond kwa sekunde 59 ikielekea dakika moja bado hakuna view hata moja ilikuwa imerekodi.
Hili lilizua mjadala w ani nani anadanganya nani kati ya Harmonize na Diamond kwani kwa kulinganisha tu Diamond yupo juu ya harmonize kwa kile kitu lakini iweje ngoma yake kwa takriban dakika moja haina view hata moja na ya yule dogo wake Harmonize kwa sekunde ishirini tu tayari views ni milioni kwenda mbele?
Unapozidi kukuna kichwa kupata ukweli wa hayo, fahamu kwamba mpaka kufikia Jumanne asubuhi, ile ya Harmonize bado ilikuwa inariyariya kwa views milioni 2.9 kwa siku sita sasa huku hiyo ya Diamond, Wonder ikiwa imepanda hadi views 934K chini ya saa ishirini na moja.