Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Natamani kwenda Marekani na Rais Samia

Samia Harmonize 95123 Harmonize: Natamani kwenda Marekani na Rais Samia

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Staa wa Bongofleva, Harmonize amesema uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusafiri nao na kuwezesha Wasanii kwenda nje ya Nchi ni mzuri ambapo amesema anaamini baada ya Wasanii wa Bongomovie kwenda Korea hata Wasanii wa Bongofleva nao watapata nafasi ya kwenda Nchi mbalimbali.

Akiongea na Waandishi wa Habari jana Julai 10, 2024 Jijini Dar es salaam wakati akiitambulisha mchezo wake mpya wa Kubashiri wa Bukua Milioni, Harmonize amesema “Rais kuja kwenye uzinduzi wa Album yangu sio kwasababu yangu tu ni kwasababu Rais anatupenda Wasanii.

“Mimi natamani kwenda nje, na ofcourse lazima nitaenda nje na ukiuliza Nchi gani nitakuambia tudondoke state hapo (Marekani), Madam (Rais Samia) tupeleke zetu state, mpigie simu Mzee Biden mwambie nakuja na Vijana akina Jay Z tuwakute pale tuzungumze, si umeona akina steve wanazungumza na Wakorea.

“Mimi najua itafika wakati wa kwenda Wasanii wa Bongofleva na tutafurahi sana kama walivyofurahi Wasanii wa Bongomovie, tupo kwenye foleni yeyote atakayebahatika kwenda atakuwa ametuwakilisha wote.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live