Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H Baba amkingia kifua Harmonize

H BABA.png?fit=712%2C372&ssl=1 H Baba

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harmonize ndiye msanii kinara atakayetumbuiza kwenye Tamasha la Pamba Day leo Jumamosi litakalofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, huku H.Baba akimkingia kifua msanii huyo na kuwatoa wasiwasi mashabiki akisema atawapa burudani ya uhakika kuliko aliyoitoa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Mbali na Harmonize na Dullah Makabila, tamasha hilo ambalo litahitimishwa na mchezo wa kirafiki kati ya Pamba Jiji dhidi ya Vital’O ya Burundi utakaochezwa saa 10:00 jioni, katika burudani watakuwepo pia wasanii wenyeji wa Mwanza kama Fid Q, H.Baba, Kala Jeremiah, Vanillah, Baraka Da Prince, Mo Music, Bob Haisa na Sajna.

H.Baba aliyewahi kufanya kolabo na Harmonize kwenye Wimbo wa ‘Attitude’ wakiwa na Awilo Longomba, amesema kwa sasa ana ushirikiano mzuri na Harmonize, hivyo matumaini yake atafanya shoo nzuri na kuwapa burudani wana Mwanza.

"Tumetoka kifungoni, sasa tumerudi, amini kwamba hii ni Pamba mpya, sisi wasanii tumejipanga, Mwanza hatuna uropokaji bali ni watu wa vitendo,” amesema H. Baba na kuongeza.

“Naamini Harmonize atafanya kitu kizuri na furaha yetu kila msanii atafanya vizuri, alichokifanya kule (Wiki ya Mwananchi) atafanya vizuri zaidi hapa Mwanza, tutashirikiana naye pamoja tunaamini tutafanya shoo nzuri na kuwapa furaha Wana Mwanza.”

H.Baba ambaye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya Pamba Jiji FC, amewakosoa wasanii wanaotunga nyimbo za timu bila kuwa na ujumbe wowote na kuishia kutaja majina ya wachezaji, viongozi na makocha, huku akisisitiza kuwa furaha ya timu ni kutengeneza wimbo kwa ajili ya timu.

Ikumbukwe kwamba, Harmonize alitumbuiza katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi ambalo ni la Klabu ya Yanga lililofanyika Agosti 4, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambapo shoo yake ilikosolewa na watu mbalimbali wakidai hakufanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live