Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H.Baba: Naishi kwa uwezo wa Mungu na Diamond

Diamond H Baba H.Baba na Diamond

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Hamisi Baba ‘H.Baba’ amesema yeye anaishi kwa uwezo wa Mungu na Diamond Platnumz pekee.

H.Baba ambaye ni chawa wa Diamond amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akimmwagia sifa kibao CEO huyo wa WCB kwa kumwajiri na kufanya maisha yake yaende.

“Asante sana Diamond Platnumz, nitaendelea kukushukuru nina kila sababu ya kukushukuru. Kwanza nimepata mwaliko mkubwa nchini Marekani tar 18/05/2023, hii yote ni kwa ajili yako, asante sana una moyo wa kipekee, sijaona moyo huo kwa sisi vijana, uwe billionaire kijana kama Diamond tungeambulia makofi na dharau.

“Umenipa ubalozi wa mwaka mzima kila mwezi nachukua Tsh milioni 4, nakueshimu, hii kwangu ni heshima kubwa, naishi nasaidia familia yangu Mwanza na Dar kwa ajili yako. Nakushukuru sana familia inaenda chooni. Nikushukuru kidogo kwao kikubwa kwangu familia yangu inakushukuru wana-Mwanza wanakushukuru.

“Naishi kwa uwezo wa #Allah na #Diamond. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu pia akupe mwisho mwema. Kiukweli nafasi ulionayo Naseeb angeipata msanii mwingine tofauti nawewe tungekoma hapa mjini, wangetembea bila nguo kiburi cha fedha.

“Angalia billionaire kijana Diamond umetulia unasaidia watu wengi umeajili vijana kibao na mimi ndani ata siringi. Mungu pekee, Naseeb pekee kimbilio langu H.Dangote," amesema H.Baba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: