Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fancy Fingers wa Sauti Sol Atoka Kivyake

Video Archive
Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fancy Fingers wa Sauti Sol atoka kivyake

MEMBA wa Kundi la Sauti Sol la nchini Kenya, Fancy Fingers ambaye ni mtayarishaji wa muziki, ameachia singo yake inayokwenda kwa jina la “How I Met Your Mama” akiwa kama solo artist.

Hii ni ishara ya mwanzo wake mpya wa safari yake binafsi kama mburudishaji na mwimbaji wa pekee.

Wimbo huo, ambao pia upo kwenye video, umeandikwa, kuimbwa na kutayarishwa na Fancy Fingers – ni wimbo maalumu kwa mwanaye ambapo ameamua kutoa yake ya moyoni kwa mwanawe kusimulia hadithi ya maisha halisi, inayoelezea jinsi alivyokutana na mama yake.

Kabla ya kuachia kibao hicho, Fancy Fingers anasema: “Wimbo huu ni muunganiko wa sauti za Wakenya na Warundi, ambao unamwonyesha mwanangu asili yake. Kwa sababu hiyo ni sehemu ya utambulisho wake.”

Anaongeza: “Tunahitaji kusimulia hadithi za Kiafrika kwa vijana wetu. Nilichagua kuanzia jinsi nilivyokutana na mama wa mwanangu, mke wangu. Mazungumzo na marafiki zangu pia yalithibitisha kwamba wengi wetu hatujui hadithi kamili ya jinsi wazazi wetu walivyokutana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live