Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu safari ya maisha Dimpoz na Diamond na urafiki wao

Mondi Dimpoz (1).jpeg Diamond na Dimpoz.

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Omary Nyembo maarufu kam Ommy Dimpoz amefunguka hustles alizopitia akiwa na rafiki yake Diamond Platnumz wakati wakitafuta tobo la kutokea walipokuwa wakianza sanaa ya muziki.

Dimpoz anatupitisha kwenye simulizi fupi ya maisha na ushikaji wao na CEO huyo wa Lebo ya WCB ambaye kwa sasa hakuna ubishi ndiye staa wa muziki namba moja Bongo.

“Nakumbuka siku moja nimekwenda kwao pale Tandale nikamkuta ameweka soda mbili anakunywa, nikamuuliza kwa nini unakunywa soda mbili akasema zama nilikuwa nashindwa hata kununua soda moja mpaka nimwombe mtu animiminie kwenye kikombe, sasa hivi naweza kununua si bora ninywe zote tu, nikasema huyu jamaa ana hasira na maisha, kwa hiyo wakati mwingine ukiona watu wanaendesha hizi Rolls-Royce inabiri uwaheshimu tu wametoka mbali.

“Mwanzoni alikuwa na kipikipiki kwenye kilima inabidi nishuke, nyuma ya kile kipikipiki kulikuwa nan a kama kikabati anaweka poda, mkifika sehemu lazima apake poda kwanza halafu ndio mtaingia sehemu.

“Kuna wakati akaja kununua kigari hakina AC, akanipitia nyumbani ananiambia nibebe shati anasema kuna sehemu tukifika hatuwezi kutembea tukajidharaulisha kwa kuacha gari vioo wazi kisa hakuna AC, kwa hiyo tutafunga vioo kisha tukishuka kama tumelowana jasho tutabadilisha mashati tutaendelea na mitikasi yetu.

“Siku moja tukaenda kituo cha kujaza mafuta akatoa tsh 50000 akasema nimwambie jamaa aweke mafuta ya Sth 4,000 heti buku ya kulaza gari parking, nikamwambia siwezi, mwambie yeye huyo muuzaji ni aibu,” amesema Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: