Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Esma apigwa na wezi wa mtandaoni

Esma Nms Esma apigwa na wezi wa mtandaoni

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dada wa msanii Diamond Platnumz @_esmaplatnumz, ameoneshwa kusikitishwa na vijana wezi waliyotumia simu yake kumuibia pesa kwa njia ya kimtandao.

Kupitia ukurusa wake wa instagram Esma Platnumz ameandika ujumbe huu "Habari ndugu zangu, kiukweli hakuna kitu nimeumia kama kuifanya huruma yangu kuwa na malipo ya kuibiwa na vijana wadogo sana kwa macho ya haraka hata sasa hivi nikisema niwakamate ni kuwapa shida wazazi wao na familia zao.

"Juzi walikuja watu dukani kwangu hawa wanao sajili laini walikuwa watatu wa dada wawili mmoja mjamzito na mkaka mmoja, kwa kuwa nilikuwa na shida kwenye laini yangu nikaomba wanisaidie kunifanyia marekebisho kwenye bundles sikuwa na shaka kabisa sababu kwa jinsi walivyokuwa wamevaa niliweka imani kabisa ni wakala wa mtandao sikuwa na shida kabisa, ajabu wale vijana wakafanya wanayojua wao kisha wakaondoka.

"Sikuwa na shaka kabisa na vitambaa niliwapa wale wadada kwa huruma kama nilivyosema mmoja wao alikuwa mjamzito, jana usiku sasa niko nyumbani nikaona text zinaanza kuingia kwa fujo kuja kutahamaki kumbe walichukua namba yangu ya siri na kwa mujibu wa @vodacomtanzania majibu niliyopewa ni kwamba wale vijana wame download app ambayo imewaruhusu kuingia kwenye mpesa yangu na kujitumia pesa zangu pamoja na kunikopea mikopo ambayo sijawahi hata siku moja kukopa.

"Nimeumia sana sikutegemea kama vijana wale wangeweza kufanya hiki walichofanya ila nimemuachia mungu leo wamefanya kwangu kesho wataendelea kufanya kwa wengine naomba tuwe makini sana na usiwaamini hawa vijana wanaopita na kusema wanafanya usajili wa laini ni wezi watupu na makampuni ya mitandao mzingatie hili vijana wenu wanafanya mambo ya ajabu huku mtaani wanatuibia kazi ambayo mnawapa wanakuja kufanya vitu tofauti ni wezi wezi wezi na tunapaswa kuwapinga kwa sauti kubwa ni wezi watupu.

"@vodacomtanzania vijana wenu huku mitaani ni wezi wezi wezi na tunaomba mlifanyie kazi hili watu wanaibiwa sana."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live