Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eddie Murphy aoa baada ya miaka sita ya uchumba

Murphy Eddie Murphy aoa baada ya miaka sita ya uchumba

Sun, 14 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji kutoka nchini Marekani, Eddie Murphy amefunga ndoa na mpenzi wake wa Paige Butcher baada ya kudumu mika sita kwenye uchumba.

Inaelezwa kuwa wanandoa hao waliokuwa kwenye uchumba kwa takriban miaka miaka sita, walifunga ndoa katika sherehe ya faragha iliyojumuisha familia na marafiki wachache wa karibu.

Hata hivyo harusi ya wawili hao ilfanyika Julai 9, akitka kijiji cha Anguilla kwenye visiwa vya Caribbean.

Eddie Murphy mwenye umri wa miaka 66 na mke wake mwanamitindo wa kutoka nchini Australia, Paige Butcher, mwenye umri wa miaka 44 waliingia kwenye uchumba mwaka 2018.

Mwigizaji huyo amewahi kufanya filamu kama, Trading Place, Tower Heist, Boomerang, Coming 2 America, Beverly Hills Cop III, Norbit na nyingine nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live