Mchekeshaji Ebitoke amefunguka ukweli wa tetesi za kutoka kimapenzi na Boss wake.
Hapo awali tuhuma za Ebitoke kutoka na Boss wake zilivumishwa na dada maarufu mtandaoni, Mange Kimambi.
“Si kweli nilikuwa natembea na Boss wangu, Watanzania wanielewe tu jamani. Kwenye ugomvi wao labda mimi naweza nikawa sababu lakini si kwamba natoka na Boss wangu, Sijakosana na Mamaa Ashura, huwenda ikawa wao kwa wao,” Ebitoke ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Ebitoke ameongeza kuwa hivi karibuni ataanza kuonekana katika kazi mpya na Mamaa Ashura ambaye kwa kipindi kirefu hajaonekana katika kundi lao la Timamu.