Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EFM bado inaongoza kwa kusikilizwa Dar – Ssebo

Video Archive
Wed, 28 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo amefunguka kwa kuzungumzia mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha miaka 4.



Ssebo alisema hayo muda mchache baada ya kuzindua kampeni mpya ya ‘Shika Ndinga’ ambayo inaendana sambamba na sherehe za kituo hicho za kupewa leseni ya kurusha matangazo.

“Kubwa zaidi siku ya leo ni kutangaza sherehe za miaka minne ya kuzaliwa kwa kituo chetu cha Efm na tunazo sababu nyingi sana za kusherehekea uwepo wetu,Wakati tunaanza tulikuwa na wafanyakazi 10 tu lakini leo hii E-fm imeajiri wafanyakazi zaidi ya mia moja,” alisema Ssebo.

Aliongeza “Wakati tunaanza tulikuwa tunasikika Daresalaam leo hii E-fm inasikika kwenye mikoa 6 pia tumeweza kuwawezesha wadau wetu na mdau wetu mkubwa ni msikilizaji wa E-fm tukiwa na bidhaa kama Shika Ndinga ambapo tumefanikiwa kutoa magari ya biashara pamoja na bodaboda, Tunayo pia bidhaa ya Sakasaka tumeweza kutoa mitaji lakini pia bidhaa yetu ya Mchizi Wangu tumemuwezesha ‘Single Mother’ kwa kuwapatia mahitaji yao”.

Chanzo: bongo5.com