Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudubaya: Baba Levo apunguze kuropokaropoka

Dudubaya Levo Dudubaya: Baba Levo apunguze kuropokaropoka

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Dudubaya amemtaka chawa wa Diamond aache kurupokaropoka hasa kwa vitu ambavyo havina msingi.

Dudubaya amefunguka hayo juzikati alipofanya mahojiano na Bongo Five ambapo alipoulizwa kuhusu sakata la Baba Levo na Sallam kumsema vibaya P Funk, akasema wote wawili wamemkosea prodyuza huyo mkongwe.

“Wamemvunjia heshima kusema kwamba amefanya nini P Funk kwenye huu muziki. Baba Levo kumwambia unamtetea Harmonize ambaye anatembea na mzazi mwenzio haikuwa sawa. Kwani kuzaa na mtu ni tatizo?

“Akumbuke P Funk ana ndoa yake, alitakiwa kumheshimu. Kumsema vile ni kumkosea heshima,” alisema Dudubaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: