Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dr. Cheni aanika siri nzito ya Steven Kanumba

Kanumba One Cheni Dr. Cheni aanika siri nzito ya Steven Kanumba

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji maarufu nchini ambaye pia ni mshereheshaji Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' amesema kuwa siri kubwa ya mwigizaji mwenzao, Steven Charles Kanumba kufanya vizuri katika tasnia hiyo ilikuwa ni uwekezaji mkubwa alioufanya katika kazi zake tofauti na wasanii wenzake.

Dr. Cheni amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir katika kipindi chake cha Salama Na.. huku akiongeza waigizaji wengine walifanya kazi zao kwa bajeti ndogo ndiyo sababu kazi zao zilionekana kuwa chini ya viwango ikilinganishwa na zile alizofanya Kanumba.

“Mwenzetu Steven Kanumba alikuwa anaoneka yuko juu kwa sababu alipata mwekezaji kwenye kazi zake za sanaa, alikuwa anaweza kuwekeza hata Tsh milioni 20 kwa sababu mwekezaji huyo alimwambia aandike stori ya aina yoyote na achukue wasanii kutoka sehemu yoyote yeye atagharamia, ndiyo maana mlikuwa mnamuona yuko namba moja.

“Sisi video zetu zilikuwa zinathamani ya Tsh milioni mbili, ikizidi sana tano, kwa hiyo hiyo ilichangia Bongo Movie kupotea baada ya Kanumba kufariki,” amesema Dkt. Cheni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live