Mwigizaji maarufu nchini ambaye pia ni mshereheshaji Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' amesema kuwa hakuwa anafahamu iwapo muigizaji mwenzake, Elizabeth Michael 'Lulu' alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Steven Kanumba.
Dr. Cheni amesema hayo wakati akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir katika kipindi chake cha Salama Na.. huku akiongeza kuwa baada ya Lulu kukamatwa, yeye ilibidi asimame kama baba yake mzazi ili kuhakikisha anamsaidia kumtoa jela.
"Kipindi Elizabeth Michael yupo gerezani kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu na kwa mama Lulu, maana mimi nilikuwa kama baba yake na mpaka sasa Lulu ni mwanangu.
“Sikujua kama alikuwa kwenye mahusiano na Kanumba, kwa kuwa umri wake ulikuwa mdogo sana.. miaka 16 ukilinganisha na umri wa Kanumba kwa wakati huo.
“Nilivyosia yeye ndiye amemuua na miaka aliyohukumiwa nilijua anaenda kuzeekea jera, lakini Mungu alisaidia akatoka ingawa watu walitukatisha sana tamaa kuwa hawezi kutoka,"Dkt. Cheni.