Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dj Sinyorita wa Clouds Fm awajibu wasanii wanaolalamika ngoma zao kubaniwa (+video)

Video Archive
Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Dj Sinyorita ambaye mara nyingi amekuwa akisikika katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm amefunguka kuhusu malalamiko ya baadhi ya wasanii ngoma zao kutopata air time katika radio station mbali mbali.



Sinyorita ameiambia Bongo5 kuwa suala hilo inategemea na msanii husika ila muziki wa sasa Bongo una ushindani mkubwa na nyimbo kali na nzuri ni nyingi hivyo badhi nyimbo zisizochezezwa mara nyingi huwa na kasoro.

“Halafu pia Dj huwezi ukapiga nyimbo zote, nyimbo kali ni nyingi kwa hiyo inabidi uchague leo unapiga hizo kesho hizi, nyimbo kali ni nyingi za hapa na za mbele,” amesema.

“Kama msanii ngoma yako haijapigwa leo chill isipopigwa na mimi itapigwa na Dj mwingine, isipopigwa na Clouds itapigwa station nyingine,” ameongeza Sinyorita.

Kabla ya kujiunga na Clouds Fm Dj Sinyorita alikuwa akisikika kupitia East Africa Radio katika kipindi cha The Cruise.

Soma zaidi; Vuta N’kuvute: Dj Sinyorita na Mami wa EA Radio wachukuliwa 

Chanzo: bongo5.com