Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond aweka rekodi kubwa duniani - VIDEO

Diamond Komasava S Diamond aweka rekodi kubwa duniani - VIDEO

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wimbo wa msanii Nassib Abdul maarufu Diamond Platinumz wa 'Komasava' unazidi kuchanja mbunga baada ya kuingia kwenye chati maarufu za muziki nchini Marekani za Billboard na kuweka rekodi mpya.

Wimbo huo umeingia katika chati hizo leo Agosti 6, 2024 ukiwa ingizo jipya na kushika nafasi ya 39 katika kipengele cha ' Afrobeats songs Top 50'.

Jambo hilo limeufanya wimbo kuwa wimbo wa kwanza kutoka Tanzania kuingia katika chati hizo kubwa Marekani na duniani kwa ujumla wake.

Diamond aliiachia Komasava kwa mara ya kwanza miezi mitatu iliyopita, akiwa amewashirikisha wakali wawili wa 'Amapiano' kutoka Afrika Kusini Khalil Harisson na Mwanadada Chley ikiwa ni Audio.

Diamond Julai 26 mwaka huu, aliachia video ya wimbo huo ambao ulikuwa remix ndani yake akionekana muimbaji mashuhuri kutoka Marekani, Jason Derulo.

Baada ya hapo wimbo huo uliendelea kukaa katika nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki duniani hadi leo ilipotoboa hadi Billboard.

Wasanii kutoka Nigeria na Afrika Kusini wamekuwa wakitawala kwenye chati hizo na leo mwanadada Tyala kutoka kwa Madiba ndiye ameshika namba moja na ngoma yake ya Water.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live