Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Wema wamo kwenye Historia ya Yanga

IMG 20230804 WA0007 Diamond, Wema wamo kwenye Historia ya Yanga

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangaza kuwa siku ya Jumatatu Agosti 7, 2023 itazindua rasmi Documentary ya Msimu wa Kihistoria wa 2022//23 katika Ukumbi wa Sinema Century Cinemax, Dar Free Market, jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika jana Alhamisi, Agosti 3, 2023.

"Documentary hii iliyotengenezwa kwa utaalamu mkubwa na yenye hadhi ya kuonyeshwa Sinema inakwenda kuwaonyesha Wanachama na Mashabiki wetu maudhui mengi na makubwa ambayo hauwezi kuyapata sehemu yoyote," amesema Kamwe.

Aidha, katika documentary hiyo Yanga imethibitisha msanii nguli nchini Diamond Platinumz sambamba na aliyekuwa Miss Tanzania mnamo 2006, Wema Abraham Sepetu watakuwa sehemu ya tukio hilo la Kihistoria la Wananchi.

NB: DOCUMENTARY (Filamu ya hali halisi) ni picha ya mwendo (Video) isiyo ya kubuni inayokusudiwa kuandika ukweli wa kimsingi kwa madhumuni ya mafundisho, elimu, au kudumisha rekodi ya kihistoria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: