Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Ndoto yangu ni kuwa bilionea namba moja Duniani

Diamond Platnumz Wonder Video Diamond: Ndoto yangu ni kuwa bilionea namba moja Duniani

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo kwenye uzinduzi wa Wasafi Festival ametangaza kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa tajiri namba moja Duniani na anaamini ipo siku atafanikisha.

Sambamba na hilo ameeleza kuwa Mwaka huu atatambulisha Bidhaa zake mpya ambazo ameahidi zitapendwa sana hivyo anaomba watu wamuunge mkono.

"Naomba vijana wenzangu mlisikilize vizuri. Ndoto yangu kubwa kwenye Maisha ni kuwa tajiri namba moja Duniani. Na ninawathibitishia kuwa nitakuwa tajiri namba moja duniani,” alisema Diamond Platinumz.

Diamond amekumbushia kuwa hapo zamani alikuwa ana ndoto ya kumiliki Gari aina ya Rolls Royce hatimaye hivi sasa anayo, hivyo anatarajia pia kuwa tajiri namba moja Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live