Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daz Nundaz, The Bongo Flava Mountainous - 2

Daz Dundaz Ms Daz Nundaz, The Bongo Flava Mountainous - 2

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

DAZ Nundaz yenye five headliners, Critic, Ferooz, Daz Baba, La’Rhumba na Sajo, ni muunganiko wa familia kubwa inayowaleta pichani, Suwa Side, Scout Jenta, Pablo na wengine. RIP Pablo!

Mwaka 1999, Manunda wakiwa madenti, walijikabidhi kwa godfather P Funk. Walikuwa na Sh30,000, vichwani wana shairi la wimbo “Bwana Alawa”.

Manunda madenti wana vipaji vikubwa, P Funk aliwakubali. Tatizo kila walipoibuka studio kwake, Bongo Records, walishonana nyomi, studio ilifurika. P Funk aliwapa appointment ya kuwarekodia, akawaambia siku hiyo waende wahusika tu.

Siku ilipofika, Daz Nundaz walitinga Bongo Records wakiwa mtiti kama kawaida. P Funk, akaona madenti wanamzoea vibaya. Akawaambia kama wanataka kurekodi watoe Sh50,000. Ile Sh30,000 akawarudishia. Manunda wakakosa Sh20,000. Wakasepa nyuso zikifoka ndita!

Hiyo ndiyo asili ya mageuzi, kutoka Bongo Records kwenda FM Studio kwa scientist Mika Mwamba. Wakabadili channel, wakauweka kando “Bwana Alawa”, wakarekodi “Maji ya Shingo”, story ya yatima anayesoteshwa na walimwengu hadi maji yakamfika shingoni.

Jamhuri ya Muungano, dola ya Generation Z mpaka kwa Papa Seven, kila mtu aliimba “jela ni kitu gani nitakwenda nitaachiwa”. Ukimya kidogo ulifuata. Halafu wakausimamisha mwaka 2001 kwa ngoma ya uchuro. “Kamanda” ndiyo jina la track. Manunda walileta balaa kubwa. How come majanki wanajiimbia kifo halafu linakuwa pini la kila mtaa, sebule hadi subule?

Ni manunda madenti, lakini wanazungumza topic ngumu yenye kumgusa kila binadamu. Kamanda ilivuruga, mpaka klabu wana walilipuka “aamualo Mola wala hawezi-kosea, narudi undongoni nilipotokea. Uhai bado nautamani, ila sipaswi kubaki duniani.”

Makundi rika yote, wake kwa waume, mradi Kiswahili ndiyo lugha, walikubaliana one term, kwamba Daz Nundaz ni wanoma, halafu noma yao ni kipeo cha pili. Walipoachia “Barua”, kaumu ikaguna eeeh, mbona imekuwa sifa?

Yanasemwa haya kuushuhudia ukuu wa Daz Nundaz. Kila mpenda muziki, hususan Bongo Flava, tarehe kichwani ni Julai 19, 2024. Katika spot la ki-epic, Warehouse Arena, Oysterbay. Sugu The Jongwe ataongoza shughuli ya kuwasimika Daz Nundaz hadhi ya Bongo Flava Honors.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live