Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daz Dundaz, The Bongo Flava Mountainous- 3

Daz Dundaz Ms Daz Dundaz

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binadamu muungwana na mwadilifu atakuwa mtiifu jina Daz Nundaz linapotajwa. Rejea Maji ya Shingo, Kamanda na Barua. Review tungo zao, lyrics kwa lyrics. Utakubali, Daz Nundaz walikuwa wavulana, wanafunzi, lakini maarifa na hekima zao, vilizidi umri wao.

Vijana wa shule, wanaandika kuhusu mapenzi na usaliti. Ukosefu wa fedha unafanya watu wakimbiwe na wanaowapenda. Unashitukizwa tu na barua, umpendaye anafunga ndoa na mwingine, kisa huna kitu. Ni story ya wimbo “Barua”.

Pitia uwasilishaji wao. It’s masterful. Ona Chemistry; Daz Baba anamchokonoa Ferooz kilichomsibu. Ferooz anasimulia mkasa wa “Barua”. Critic anasoma barua. Ferooz anarejea kwa hisia kuomba barua isiendelee kusomwa. Inamchoma kumoyo.

Daz Nundaz ni kundi lililowafanya wahafidhina kusalimu amri, wakakiri Bongo Flava si uhuni. Kila kitu kilifanywa na wavulana watano, the powerful dreamers, waliokuwa safarini kuwa wanaume; Critic, Ferooz, Daz Baba, Sajo na La’Rhumba.

The upper hand of Daz Nundaz ni moto wao mkali wakifanya kazi pamoja, halafu kuna members wawili wanaposimama solo, kila mmoja anageuka nyangumi baharini; ni Ferooz na Daz Baba. Kazi zao nje ya kundi, zimesimenti kila ukweli kuwa Daz Nundaz ni among the GOATS of Bongo Flava.

Mchapo wa “Jirushe”, Ferooz featuring Jay Moe. “Wife”, Daz Baba collabo na Ngwair. “Starehe”, Ferooz with Prof Jay. “Namba 8”, Daz Baba kibingwa na Fid Q. Bonge la dude “Jahazi”, na wanaye wa Daz Nundaz. Kuna dubwashika linaitwa “Nipe Tano”, kazi ya Daz Baba na familia yake ya Daz Nundaz plus Suwa Side, Pablo, Scout Jentaz na wengine.

“Elimu Dunia” ya Daz Baba, siyo tu ni moja kati ya albamu bora za Bongo Flava za muda wote, bali pia wimbo wenyewe “Elimu Dunia”, ni ujumbe wa maisha kuhusu kijana aliyekata ringi mtaani. “Safari” ya Ferooz, ina rekodi ya kuwa moja ya albamu zenye matokeo makubwa sokoni.

Julai 19, 2024, haitakuwa siku ya Bongo Flava Honors kuwaheshimisha Daz Nundaz, bali kuipa Bongo Flava thamani inayostahili. Jina “Daz Nundaz” ni chachandu ya Bongo Flava. Performance ya live band kutoka kwa Manunda, mwenyeji wa shughuli, Sugu The Jongwe, makutano ni Warehouse Arena, Oysterbay.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live