Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido atangaza ajira kwa vijana wenye leseni za udereva wasio na kazi

Davido Msz Davido atangaza ajira kwa vijana wenye leseni za udereva wasio na kazi

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiachana na muziki, Davido anataka kupanua himaya yake kibiashara kwa kujitosa kwenye biashara nyingine ya tofauti kabisa tofauti na muziki.

Msanii huyo kutoka nchini Nigeria anaanzisha biashara ya huduma ya usafiri wa (Taxi kama vile Uber) kwa ajili ya kuwapa ajira vijana wa Nigeria.

Davido anashirikiana na kampuni ya CIG Motors inayouza magari kutoka China kutoa magari mengi sana kwa madereva vijana walio na leseni lakini hawana kazi

Msanii huyo anasema ni madereva wenye leseni na wasio na ajira ndio watakaopewa kipaombele.

Kwa mujibu wa CNBC Africa, magari hayo yatakayokuwa na chapa ya Davido, yanatarajiwa kuwa tayari baada ya mwezi mmoja au miwili kuanzia sasa.

Wakati huo huo, nyota huyo wa muziki wa Afrobeats anasema kujitosa kwake kwenye ujasiriamali hakutaondoa umakini wake kwenye muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live