Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Dangote: Ninakodi nyumba za kuishi

Dangote Mszzz Dangote: Ninakodi nyumba za kuishi

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tajiri wa kwanza Afrika, Aliko Dangote amewashangaza watu wengi wa Nigeria baada ya kusema hana nyumba nje ya nchi hiyo, na mara nyingi hulazimika kukodi anaposafiri nje ya Nigeria.

Kwa sasa Dangote ana nyumba mbili, moja ikiwa Kano kule alikozaliwa na nyingine ikiwa katika jiji la Lagos, Nigeria.

Katika jarida la Forbes la mwezi Januari liliamuandika Tajiri Dangote kama mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 13 mfululizo licha ya kuwepo kwa matatizo ya uchumi nchini Nigeria.

Utajiri wake uliweza kupanda kwa dola za kimarekani milioni 400 zaidi mwaka jana, na kumpa thamani ya jumla ya thamani ya dola za kimarekani Bilioni $13.9.

Kwa sasa mfanyabiashara huyo ana umri wa miaka 66 ambaye amejitajirisha kwa kuuza saruji na sukari na mwaka jana alifungua kiwanda cha kusafisha mafuta katika kitovu cha uchumi cha Nigeria, Lagos.

Hatahivyo kauli yake hii iliwashangaza watu wengi nchini humo ambapo matajiri wengi wana sifa ya maisha ya kifahari na wengi wakimiliki nyumba mjini London, Dubai au hata Atlanta.

Matamshi yake yamezua hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakisema ni uamuzi wa busara wa kibiashara kwani ni nafuu kulipa kodi kuliko kununua nyumba.

Bw Dangote alisema sababu ya uamuzi wake ni kwamba anataka kuona Nigeria inakua. "Sababu ya kutokuwa na nyumba London au Marekani ni kuwa nilitaka kuangazia ukuaji wa viwanda nchini Nigeria," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live