Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daftari lenye mistari ya Lili Wayne kuuzwa Bilioni 13

Lili Wayneeeeee Daftari lenye mistari ya Lili Wayne kuuzwa Bilioni 13

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daftari (notebook) ya zamani ya mwananamuziki Lil Wayne aliyokuwa akiitumia kuandika nyimbo zake mbalimbali lipo sokoni kwa ajili ya kuuzwa.

Kwa mujibu wa Tmz imeeleza kuwa daftari hilo la #Wayne alilokuwa akitumia kuandika mashairi yake toka mwaka 1990 sasa lipo sokoni na linauzwa dola 5 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 13 bilioni.

Hata hivyo tovuti ya Tmz imeweka wazi kuwa atakae fanikiwa kununua daftari hilo basi atakutana na mashairi ya wimbo wa We On Fire’ na ‘I Feel’ aliyoyaandika wakati yupo katika kundi la ‘Hot Boys’ akiwa na miaka 17.

Utakumbuka kuwa mwaka 2019 mwanaume mmoja alitaka kuliuza daftari hilo akidai kuwa aliliokoto, hata hivyo #LilWayne alipinga lisiuzwe kwani ilikuwa ni mali yake na hatimaye alishinda kesi mahakamani na kukabidhiwa tena daftari hilo. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live