Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DJ Seven, Harmonize wafika pabaya! DJ Seven ashusha ujumbe mzito-VIDEO

Video Archive
Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa DJ wa Harmonize, DJ Seven amemlipua kiaina Harmonize kwa kumuambia kuwa, alikuwa naye kwenye wakati wanajitafuta akiamini wakifanikiwa watakula pamoja mema ya nchi lakini mambo yamekuwa tofauti.

Licha ya kuwa hajamtaja jina moja kwa moja Harmonize lakini ujumbe huo unaonesha dhahiri amemlenga yeye kwa kuzingatia ndiye mtu waliyefanya naye kazi na sasa Harmonize yupo kwenye kilele cha mafanikio na wamezinguana.

Harmonize na DJ Seven walikuwa wakifanya kazi pamoja kabla ya kugombana na kila mmoja kushika njia zake na sasa kila mtu yupo kivyake. Bifu lao lilihusishwa pia na madai ya Harmonize kumchukua mrembo wa Seven, Poshy Queen lakini hata hivyo, Harmonize alinakanusha, Poshy pia alikanusha kuwa na uhusiano na Seven.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live