Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Caren Simba: Nawachukia wanaume ambao hawawapi fedha wapenzi wao

Careen Simba Er Caren Simba.

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa filamu ambaye kwa hivi sasa anafanya vizuri sana kupitia filamu za Kibongo na video vixen, Careen Simba amesema anawachukia wanaume ambao hawawapi fedha wapenzi wao wala hawawajali na kuwahudumia.

Ameongeza kuwa jukumu la mwanaume siku zote ni kumpa fedha mpenzi wake na anavyompa si kama anamhonga bali ni kumlinda na kumhudumia.

“Hakuna kitu ninachochukia kama mwanaume kuona kuwa kumpa pesa mwanamke ni kumhonga wakati ni jukumu lake. Kama ni mwanamke wako lazima umhudumie ingawa na yeye anatakiwa afanye kazi, siyo kila kitu mpaka amwambie mwanaume wake.

“Siku zote mwanamke mwenyewe ndio wa kujiweka kwenye nafasi unayotaka na sio mtu mwingine,hivyo ukichagua kujithamini na kujiheshimu na wengine watafanya hivyo, na kwa upande mtoto wangu ndio jukumu langu la kwanza,” alisema Careen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live