Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bony Mwaitege hajafariki Dunia - Mkewe afunguka

Bony Mwaitege Limebaki Bony Mwaitege hajafariki Dunia - Mkewe afunguka

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania, Boniface Mwaitege amekanusha taarifa zilizosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa muimbaji huyo amefariki dunia leo kwa ajali ya gari.

Akizungumza nasi leo Julai 22, 2024 Mke wa Mwaitege amenukuliwa akisema; “Bony Mwaitege ni mzima kabisa ametoka safari kutoka Kenya na amefika nyumbani salama, amepumzika.”

Baadhi ya Mitandao leo iliripoti kuwa Mwimbaji huyo amefariki kutokana na ajali ya barabarani kitu ambacho mkewe amesema kuwa ni uongo na uzushi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live