Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Binti ahitimu PhD akiwa na umri wa miaka 17

Dorothy Jean Tillman Ade6.jpeg Dorothy Jean Tillman.

Thu, 23 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binti mkazi wa Chicago, Marekani, Dorothy Jean Tillman, ameweka historia ya kipekee baada ya kupata Shahada ya Udaktari (Phd) ‘Doctorate degree in Integrated Behavioral health’ akiwa na umri wa miaka 17.

Akiwa na umri mdogo Dorothy alionekana kuwa mwenye malengo na mwamko wa kusoma, kwani katika umri wa miaka 7 kwa huku kwetu tungesema alianza kusoma elimu ya sekondari (A-level) na baadaye masomo ya ngazi ya chuo.

Alipofikisha umri wa miaka 14 tayari alikuwa ameshapata Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili.

Licha ya kuwa na mafanikio hayo Dorothy hakuridhika, alitazama mbele na kuweka lengo jingine la kupata Shahada ya Udaktari ambayo hatimaye aliipata katika Chuo Kikuu cha Taifa Arizona.

Dorothy ameipata Shahada hiyo ya Udaktari akiwa amesomea ‘Doctorate Degree in Integrated Behavioral Health' ambapo amesema alipata msukumo wa kusoma shahada hiyo baada ya kuchunguza namna unyanyapaa unavyowazuia wanafunzi wa chuo kikuu kupata matibabu ya afya ya akili hivyo akataka akasome ili awasaidie.

Dorothy amekiri kuwa kikubwa kilichomsaidia kufikia lengo na kupata Shahada ya Udaktari ni familia yake kusimama pamoja nae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live