Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Binti Mfalme ampa talaka tatu mumewe

Dubai Princess Sheikha Mahra Divorces Husband For Being Too Busy 800x450.jpeg Binti Mfalme ampa talaka tatu mumewe

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binti wa mtawala wa Dubai ametangaza kumtaliki mume wake kupitia mtandao ya kijamii. Ujumbe kutoka kwa akaunti ya Instagram iliyothibitishwa ya Sheikha Mahra binti Mohammed bin Rashid Al Maktoum ulisema anakatisha ndoa yake kwa kuandika: “Mimi natangaza talaka yetu.”

Ujumbe huo ambao ulianza kwa kusema “Mume wangu Mpendwa”, ulihitimishwa na maneno - “Ninakupa talaka, ninakupa talaka, na ninakupa talaka,” ukionekana kutumia desturi ya Kiislamu inayojulikana kama talaka tatu. Kitendo hicho kimewashtua wengi kwani si kawaida kwa Mke kumtaliki Mume.

Wenzi hao walioana mnamo April 2023 katika sherehe ya kifahari, na mtoto wao wa kwanza alizaliwa miezi miwili iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live