Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bilionea Warren Buffett atangaza hatima ya mali zake atakapofariki

Warren Buffett (15).jpeg Warren Buffett

Sun, 30 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwekezaji bilionea Warren Buffett amesema kuwa baada ya kifo chake, karibu mali zake zote zitahamishiwa kwenye taasisi ya hisani itakayo simamiwa na watoto wake watatu.

Buffett, ambaye ni mwenyekiti na mtendaji mkuu wa Berkshire Hathaway na mmiliki wa karibu dola bilioni 130 za hisa za kampuni hiyo, atafikisha miaka 94 mwezi Agosti.

Katika mahojiano na gazeti la Washington Post lililochapishwa Jumamosi, bilionea huyo alisema mchango wake mkubwa kwa Wakfu wa Bill & Melinda Gates (BMGF) utafikia kikomo baada ya kifo chake. "Wakfu wa Gates hauta pata pesa kutoka kwangu baada ya kifo changu," alisema.

Tangu 2006, wakati Buffett alipoamua kutoa sehemu ya mali yake kwa hisani, BMGF imepokea dola bilioni 39.3, kulingana na tovuti yake.

BMGF ilianzishwa mwaka 2000, na imekuwa moja ya mashirika makubwa ya kutoa misaada duniani. Taasisi hiyo inasema kuwa malengo yake makuu ni kuboresha huduma za afya na kupunguza umaskini uliokithiri duniani kote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live