Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bila Milioni 8, hupati viatu hivi..!

Kwantroooo Bila Milioni 8, hupati viatu hivi..!

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika ulimwengu wa mitindo, Alexander McQueen ameendelea kuliteka soko kwa ubunifu wake wa kipekee, ambapo awamu hii amezindua viatu vyenye muundo wa kwato “Hoof Boots”, vinavyouzwa dola 2,990 zaidi ya Sh 8 milioni.

Viatu hivyo ambavyo vinaelezwa kuwa vimetengenezwa kwa ngozi ya ndama, na kuwekewa mtindo wa kwato za farasi vinaenda kuwa moja ya bidhaa fasheni zenye bei ya juu.

Kutokana na muonekano wa viatu hivyo wadau mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kupongeza ubunifu huo huku wengine wakionesha kushangazwa na gharama zake licha ya kuwa wamekubali kuwa ni mtindo wa kipekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live