Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Nilimwambia Diamond amfukuze Mwijaku

Mwijakuu Na Baba Levoo Baba Levo: Nilimwambia Diamond amfukuze Mwijaku

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva na Chawa Promax wa Diamond Platnumz, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo amesema kuwa kwa sasa amekataa kufanya kazi na rafiki yake Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku kutokana na tabia za chawa mwenzake huyo.

Baba Levo amedai kuwa sababu kubwa ya kutofanya kazi na Mwijaku ni kutokana na maneno yake ya shombo na kuwachafua watu hata bila kuwa na uhakika na taarifa zake.

"Mimi sikubaliani na kile anachokifanya Mwijaku. Mimi ndiyo nilikaa na Diamond Platnumza nikamwambia anachokifanya Mwijaku sioni kama ana chuki na wewe, akapewa mkataba wa mwaka mzima na Wasafi Bet akasafirishwa mpaka Qatari.

"Juzi nilimwambia Diamond mfukuze Mwijaku kwa sababu habadiliki. Hata watu ambao anafanya nao kazi wanampa matangazo anawasemea viztu vya uongo na kuwachafua. Sina muda wa kujadiliana nae.

"Nimekaa na Mwijaku mara nyingi, ninasafiri naye namwambia ndugu yangu haya mambo unayoyaongea hakikisha yanakuwa na mantiki, usiongee tu ilimradi kumchafua mtu, ongea kitu hata ukihojiwa uwe na majibu ambayo yamenyooka.

"Mimi na Mwijaku tulikubaliana tuwe wehu tupate pesa, lakini naona mwenzangu kama anataka kuwa mwehu kweli. Juzi tulifanya kazi Zanzibar kwa sababu ilikuwa kazi ya Serikali baada ya hapo kila mtu anashika njia yake.

"Tumebakiza mkataba mmoja wa kampuni moja ambao tunafanya kazi pamoja, ni kwa sababu tulisaini mkataba mrefu kidogo.

"Makampuni mengi nimekataa kufanya kazi naye pamoja na kampuni nyingine ilipogundua wakiniambia wanataka tufanye kazi pamoja nitakataa, wakanificha wakanisainisha peke na yeye peke yake, nilipogundua nikarudisha pesa ni Tsh milioni 37 kwa sababu sioni kama anatenda haki," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: