Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo, Mwijaku kimeuamana tena

Baba Levo Na Mwijaku Tenaa Baba Levo, Mwijaku kimeuamana tena

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Baba Levo ameingilia ugomvi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kati ya msanii Diamond Platnumz na Mwijaku unaohusu nani anayemiliki pesa nyingi kuliko mwingine.

Hii ni baada ya Diamond kusema kuwa malengo yake ni kuwa bilionea namba moja duniani, jambo ambalo lilimuinua Mwijaku na kudai kuwa Mondi hana pesa wala hawezi kumfikia Fred Vunjabei.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Baba Levo ameweka ujumbe unaosomeka hivi; "Ukweli ni kwamba Fred hajamtuma kichwa mviringo kuyaongea hayo! Ukweli ni kwamba kwa sasa Fred hana hiyo nguvu ya kuvutana mashati na Lukuga naamini itamtoa kwenye mchezo na malengo yake yakujiweka sawa kimaisha.

"Kumbukumbu zangu zinaonyesha ni mimi ndio niliyeenda kumuombea msamaha kuchwa mviringo kwa Fred baada ya Fred kumfungulia kesi kichwa mviringo. Baada ya kumkashifu na kumsingizia kwamba Fred anafanya biashara haramu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live