Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Cassper Nyovest, S2kizzy awavutia pumzi Wizkid na Future (+video)

Video Archive
Fri, 9 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Producer Skizzy kutoka Switch Music Group (SMG) amesema wasanii wakubwa ambao anatamani kufanya nao kazi kwa sasa ni Wizkid kutoka Nigeria na Future kutoka Marekani.



S2kizzy ameiambia Bongo5 kutokana na kazi alizofanya na watu ambao anafanya nao kazi kwa sasa anaamini atapata connection ya kuwafikia wasanii hao.

“Msanii ambaye natamani kufanya naye kazi Afrika ni Wizkid kwanza ni msanii crazy anapenda muziki mzuri, nimemfuatilia nimeona naweza kufanya naye vitu vizuri sana, pia kwa nje mtu kama Future natamani kufanya naye kazi, ni watu ambao nawakubali,” amesema.

“Connection nimepata kutokana kuna baadhi ya watu nimeshafanya nao kazi, wasanii kama Nasty C, kina Patoranking, Cassper Nyovest, nimefanya na mtu kama Mayorkun ambaye ni mwanae Davido, kwa hiyo connection inakuwa siku baada ya siku,” ameongeza S2kizzy.

S2kizzy ni miongoni mwa ma-producer walioshiriki katika albamu ya Vanessa Mdee ‘Money Mondays’ ambapo ameisuka ngoma inayokwenda kwa jina la Pumzi ya Mwisho ambayo Vanessa kawashirikisha Cassper Nyovest na Joh Makini.

Chanzo: bongo5.com