Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Azikwa baada ya siku 579 tanfu afariki, mke wake aliamini atafufuka

The Funeral Of Siva Moodley 579 Days After He Died Picture Facebook.jpeg Azikwa baada ya siku 579 tanfu afariki, mke wake aliamini atafufuka

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Je, Wajua? Mchungaji Siva Moodley wa Afrika Kusini, alifariki Agosti 15, 2021, lakini mwili wake ulizikwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kukaa siku 579 kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, kwa sababu familia yake na waumini wa kanisa lake walikuwa wamkiamini atafufuka.

Kabla ya kifo chake Siva Moodley yeye mwenyewe alikuwa akiamini kwamba watu wanaweza kufufuliwa.

Alifariki baada ya kuugua, hata hivyo katika hali ya kushangaza badala ya kufanya matayarisho ya mazishi familia yake iliuacha mwili huo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti wakingoja afufuke.

Mke pamoja na ndugu wa marehemu walikuwa wakienda kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kumuombea kila wakati ili azinduke, lakini waliacha kwenda mahali hapo kwa miezi kadhaa na walikuwa hawapatikani kila walipotafutwa, jambo lililomlazimu mmiliki wa chumba cha kuhifadhia maiti kulifikisha jambo hilo mahakamani.

Baada ya vuta nikuvute nyingi za kisheria hatimaye Machi 16, 2024, mwili wa Siva Moodley ulizikwa kwenye makaburi ya Westpark jijini Johannesburg, mbele ya ndugu zake na familia yake lakini mke pamoja na watoto wake wawili hawakuhudhuria maziko hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live