Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Azam Media waamriwa kumlipa sh milioni 100 Mzee wa Maspatasapta

0015Mzee Wa Maspatasapta Mzee wa Maspatasapta

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, iliyoko jijini Dar es Salaam imeiamuru kampuni ya Azam Media Group Ltd kumlipa kiasi cha shilingi milioni 100 mpishi maarufu nchini Master Chef Fred Uisso maarufu kama ‘Mzee wa Maspatasapta’ baada ya kushinda kesi dhidi yake na wenzake watatu baada ya kampuni hiyo kumtangaza mpishi huyo kupitia channel yake ya Sinema Zetu kipindi kinachorushwa na Azam TV

Matangazo hayo yaliyorushwa kwa zaidi ya wiki mbili katika kipindi cha mwezi Agosti, 2023 yalionesha kuwa mpishi maarufu huyo atahudhuria katika tamasha la 'Wapi muziki na misosi Festival 2023' lililoandaliwa na EX-Nihio Ltd kampuni inayomilikiwa na Paul Mashauri

Mpishi huyo maarufu anayemiliki mgahawa wake wa vyakula vya asili uliopo Kijitonyama, aliifikisha kampuni ya Azam Media Group Ltd Ex-Nihio pamoja na Paul Mashauri katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa madai kwamba wadaiwa hao wameupotosha umma kwa kuwahadaa kuwa atashiriki katika tamasha hilo suala ambalo si la kweli

Katika Mahakama ya Kisutu Master Chef Fred Uisso aliiomba Mahakama kuwataka wadaiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kwa kuwa matangazo yake yaliuhadaa umma suala lililopelekea kukosa biashara katika mgahawa wake

Hivyo, Mahakama baada ya kusikiliza shauri hilo kwa takribani mwaka mmoja Agosti 16.2024 imefikia maamuzi kwa kuwataka washtakiwa kumlipa fidia ya madhara ya jumla kiasi cha shilingi milioni mia moja (100,000,000/-) pamoja na gharama za uendeshaji wa shauri hilo

Itakumbuka pia, Agosti 25.2023 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ilizuia kutofanyika kwa tamasha hilo baada ya Master Chef Fred Uisso kufungua shauri la kuzuia kufanyika kwa tamasha hilo la 'Wapi muziki na misosi 2023 Festiva' lililopagwa kufanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es Salaam

Akizungumza Wakili Ferdinand Makore aliyemuwakilisha mdai, mara baada ya kutoka Mahakamani hapo, amesema:

“Haya maamuzi ya leo yanatoa fundisho kwa watu wote wanaopenda kutumia majina ya watu kwa ajili ya umaarufu wa majina hayo, kwa kuwaaminisha umma kuwa fulani atakuwepo, suala ambalo mara nyingi huwa ni uongo na hufanya hivyo kwa lengo la kupata watu wengi” -Wakili Makore

"Mahakama imetamka wazi kuwa neno fulani atakuwepo bila kupata ridhaa yake kabla ya tangazo husika ni kosa kisheria” -Wakili Makore.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live