Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aunt Ezekiel azungumzia Wema Sepetu kuachwa miaka 10 ya Diamond Kigoma

Video Archive
Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Msanii wa filamu nchini Tanzania, Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa mrembo Wema Sepetu, amezungumzia kukosekana kwa mrembo  huyo katika safari ya miaka kumi ya Diamond mkoani Kigoma.

Safari hiyo ya Diamond imeanza leo Jumamosi, Desemba 28 2019 ambapo ameongozana na mashabiki zake na watu wake wa karibu huku wakitarajia kufika kesho Jumapili jioni.

Pamoja na kuwapo kwa wasanii wengi ambao baadhi yao Diamond alikiri kuwa na mchango katika muziki wake, mashabiki mitandaoni walihoji vipi kuhusu Wema kutoalikwa na kueleza kuwa alistahili.

Mashabiki wanakuja na kauli hiyo kutokana na mrembo huyo kuwahi kuwa katika mahusiano na Diamond wakati akiwa anaanza muziki.

Kutokana na matakwa hayo ya mashabiki, Mwananchi ilimuuliza Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu na Wema kutaka kujua namna alivyojisikia baada ya kuona maoni hayo ya mashabiki.

Katika maelezo yake, Aunt amesema suala la Diamond kumualika Wema au kutomualika ni uamuzi wake mwenyewe na hakuna anayeweza kumlazimisha.

"Huwezi kufanya kila jambo wanalolitaka watu, hata kama kweli mashabiki wanaona Wema alikuwa na mchango kwenye muziki wa Diamond lakini mwenyewe ndio hivyo kaamua huwezi kumlazimisha," amesema Aunt.

 

Hata hivyo, alipoulizwa kama kuna ushauri wowote huwa anampa Diamond kuhusiana na Wema, Aunt amesema hawajawahi kukaa na kumzungumzia mrembo huyo kwa kuwa walishaachana na kila mtu ana maisha yake kwa sasa.

"Naanzaje kumzungumzia Wema kwa Diamond wakati najua ana mwanamke wake kwa sasa ambaye watu wote wanamjua, nadhani sipaswi kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu ana maisha yake kwa sasa hivyo  nikifika kwa Diamond nitazungumza yanayotuhusu sisi, vilevile nitafanya hivyo kwa Wema," amesema Aunt.

Katika safari hiyo mbali na mashabiki zake, Diamond ameongozana na familia yake akiwamo mzazi mwenzake Tanasha Donna na mtoto wao, Dada zake Esma Platnumz na Queen Darleen.

Chanzo: mwananchi.co.tz