Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aslay amlilia Mzee Pembe

Aslay X Pembe Aslay amlilia Mzee Pembe

Mon, 21 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa bongo fleva Aslay, ameungana na tasnia nzima ya burudani na wadau mbalimbali kuomboleza kifo cha muigizaji mkongwe nchini maarufu kama Mzee Pembe aliyefariki dunia Octoba 20, alishiriki kwenye video ya wimbo wa Aslay 'Naenda Kusema' ambapo alikuwa ameigiza kama baba yake Aslay mwenye sifa ya kupenda na kujali michepuko kuliko familia yake.

@aslayisihaka kupitia instagram account yake ametoa maneno ya huzuni akionyeshwa kuhuzunishwa na msiba huo "Moja kati ya watu waliotengeneza barabara ya maisha yangu ya mziki ni huyu mzee PEMBE Nimepokea kwa masikitiko makubwa kwa taarifa cha kifo chake. Nungu ailaze Roho ya Marehemu Mzee wetu PEMBE mahali pema peponi pole ziwaendee familia yake na wapenda burudani wote".

Mzee Pembe ameacha pengo kubwa na atakumbukwa kwa mchango wake kwenye ukuwaji wa tasnia ya maigizo hasa vichekesho maana mzee huyu aliwafungulia njia wachekeshaji wengi wa kizazi hiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live