Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayemremba Diamond Mungu anamuona

Diamondplatnumz 277704250 124373763396008 1989015863575318023 N 1 Diamond Platnumz

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KUNA wakati huwa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz anashambuliwa kutokana na aina ya misuko ya nywele ambayo hufananishwa na mwanamke.

Si Diamond au Mondi tu aliyewahi kupitia hali kama hiyo, lakini hata wasanii wa kiume kwenye lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) kuanzia enzi za Harmonize, Rich Mavoko waliojiengua kisha Rayvanny, Mbosso na Lava Lava nao wamekuwa wakishambuliwa kutokana na tabia hiyo ya kusuka misuko ya jinsia ya kike ikiwemo twende kilioni.

Kama kawaida, Diamond anapofanya jambo f’lani, basi picha zake mpya zikumuonesha kwenye mwonekano wa kijana wa Kiislam anayekwenda kuoa zinadaiwa kufikirisha mno kiasi cha aliyemremba kuambiwa; ‘Mungu anamuona!’

Picha hizo zinadaiwa kueditiwa (filter) mno kiasi cha kuvuka mipaka na kuonekana mwenye ngozi nyororo na mrembo kwelikweli.

Picha zinadaiwa kueditiwa hadi anakuwa kama mwanamke mrembo na kinachomfanya aonekane mwanaume ni hayo madevu ambayo ameanza kufuga siku za hivi karibuni.

Wengine wanadai kwenye picha hizo amepakwa hadi lip-shine midomoni hivyo kuibua minong’ono kwamba anakoelekea siko au anayemfanya hivyo anampeleka kusikojulikana.

Kibaya zaidi, inasemekana Diamond akifanya jambo huwa kuna vijana wengi mtaani wanamuiga hivyo usishangae muda si mrembo vijana wengi wa kiume nao wakaanza kuwa na muonekano wa ‘kirembo’.

Kuna wanaotania kwamba, Diamond anachangia kupotea kwa viumbe wanaume kwa sababu wengi wanajiremba kiasi kwamba inakuwa ni ngumu kuwatofautisha na dada zao!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: