Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ally Kamwe kubeba mke wa Mwijaku wafikia hapa

Mwijaku Kamwe Mz Ally Kamwe kubeba mke wa Mwijaku wafikia hapa

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe alikuwa ameandaa watu wake kwa ajili ya kwenda kumchukua mke wa Mwijaku ambaye aliahidi kuwa iwapo Simba atafungwa na Yanga basi atampa Kamwe mke wake.

“Ndugu Waandishi kwanza niwaombeni msamaha kwasababu hili jambo limegusa hisia za Watanzania, imenichukua nusu saa kumsihi Kijana wangu (Kamwe) kwa niaba ya Wazee wa Yanga, Ally alikuwa sahihi akachukue yule mke (Alice) kwa matamshi ya yule Bwana Mdogo (Mwijaku) lakini tukiangalia thamani ya utu wa Mwanamke na Ubinadamu sio jambo sahihi yeye kama amemchoka yule Mwanamke ni bora angemwandikia talaka amuache tu.

“Sio ubinadamu kumuweka bondi au utumwa Binadamu mwingine haipo tena, tunayasema haya iwe fundisho kwa Mwijaku na Wazazi wake, Mimi ningekuwa Mzazi wa yule Binti ningejua hatua gani nachukua moja taratibu za kisheria, mapenzi yako na Club yako usimgeuze Mke kama chambo kuleta haya katika Jamii.

“Niwaombe Wapenzi wa mpira hasa Mashabiki wa Simba ikitokea tena hakutokuwa na msamaha, Ally ana thamani kubwa ya Club ya Yanga na Utanzania wake na hadhi yake kama Mwanaume unaposema nakupa Mke wangu maana yake unaona hana uwezo wa kummiliki jambo sio sahihi, atakayerudia hakutokuwa na msamaha.

“La mwisho nikuombe Kijana wangu (Kamwe) Mwanaume amepewa sifa mbili kuwa na busara na hekima, unayotumia hapa ni hekima ili kumrudishia thamani yule Mwanamke, sisi Wazee tumemzuia Kijana wetu na niwaombe Wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye kuchukua mwali wetu sisi tumesitisha,” amesema Mzee Msumi kwa niaba ya Wazee wa Yanga.

“Wapenzi wa Yanga nafikiri mmesikiliza hapa hekima za Wazee wetu, tulishajiandaa magari zaidi ya 20 yapo hapa, magari yalipambwa lakini mmesikiliza hekima za Wazee wetu, Mzee amenisihi thamani ya Mke, Mimi sipo kwenye ndoa lakini Mzee yupo kwenye ndoa muda mrefu Mimi nimemuelewa naomba tumsamehe, kwa hili la leo tumemsamehe Mwijaku.

“Tumemsamehe sio kwasababu ya akili zake ila ni kwa kuheshimu thamani ya yule Dada, ni bahati mbaya tu yule Dada ameenda kuolewa na Mwehu, sisi ni Watani wa jadi tunaweza kutaniana vitu vingi sana lakini tusivuke mipaka na kupoteza heshima na utu wa Mtu, tutaniane wenyewe kwa wenyewe, naamini hili la leo litakuwa mwisho , kama unataka kujitoa jitoe wewe tutakupokea lakini usimuhusishe Mtu mwingine.

“Leo naamini tumetoa fundisho kwake Mwijaku na Mashabiki wengine wa mpira kujiheshimu pale wanapoongea mbele ya Waandishi wa Habari au mbele za Watu kuhusu hivi vilabu viwili, hakuna anayemuogopa Mwijaku, sisi tulipanga tukaweke kambi pale wangerudi usiku tungechukua Mke na yule mbwa,” Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: