Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Aliyetumia Pesa za Kampuni kula Bata, ahukumiwa miaka mitano Jela

FotoJet 64 2 Barbara Furlow-Smiles

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Meneja wa programu za Facebook, Barbara Furlow-Smiles, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya wizi wa zaidi ya dola 5 milioni kutoka kwenye kampuni hiyo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Hukumu hiyo ilitangazwa rasmi na Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani Ryan K. Buchanan siku ya Jumatatu wiki hii..

Shughuli hizo za ulaghai Barbara alianza kuzifanya wakati wa utumishi wake kama Mtendaji Mkuu wa DEI Facebook, ambapo alianza kazi katika kampuni hiyo mwaka 2017 hadi 2021.

Aidha Desemba mwaka jana mwanadada huyo alikiri kosa na kueleza kuwa alitumia fedha hizo kuendesha maisha yake ya kifahari aliyokuwa akiishi #California.

Waendesha mashitaka walieleza kuwa Furlow-Smiles alitekeleza utapeli huo kwa kufanya malipo kwa niaba ya Facebook kwenda kwa marafiki na ndugu, pamoja kutoa huduma ambazo hazikutolewa kwenye kampuni hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live