Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Miss Afrika Kusini ashinda Miss Universe

Chidimma Adetshina 4 Aliyejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Miss Afrika Kusini ashinda Miss Universe

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlimbwende Chidimma Adetshina aliyelazimika kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Miss Afrika Kusini kutokana na utata juu ya uraia wake, ameshinda taji la Miss Universe Nigeria.

Adetshina (23), mwenye uraia wa Afrika Kusini na ambaye baba yake ni Mnigeria, alijitoa kwenye Mashindano akiwa amefikia hatua za mwisho.

Ushiriki wake nchini Afrika Kusini ulizua gumzo kubwa huku baadhi ya raia wa nchi hiyo wakiwemo Viongozi wakimpinga kutokana na asili yake.

Adetshina aliamua kujitoa kwenye Mashindano hayo kwa kile alichokitaja kuwa ni kwa amani na ustawi wake na familia yake.

Waandaaji wa Miss Universe Nigeria waliokua wakifuatilia kwa karibu utata huo, walimualika kushiriki mashindano yao.

Sasa mrembo huyo ataiwakilisha Nigeria katika mashindano ya Miss Universe yanayotarajia kufanyika mwezi Novemba nchini Mexico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live