Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba: Diamond apewe maua yake

Alikiba Diamond (1) Alikiba: Diamond apewe maua yake

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Ali Kiba amempongeza msanii mwenzake, Diamond Platnumz kwa kufanya muziki mzuri na kupenya kimataifa jambo ambalo amesema limeiheshimisha Tanzania kwenye ulimwengu wa sanaa hiyo.

Kiba amesema hayo baada ya wimbo wa Coma Sava wa Diamond ku-tend katika maeneo mengi ya Dunia mpaka kumfikia supastaa wa pop duniani, Chris Brown ambaye alijirekodi akicheza wimbo huo.

“Nimefurahishwa na inaonesha kwamba kuna namna ambavyo unaweza kufanya kitu na kikawafurahisha watu. Kipindi hiki Diamond amefanya kitu kizuri na anafanya vitu vizuri lakini hiki kimewagusa watu sana.

“Sijui imekuwaje lakini hata mimi nimefurahi sana kuona Chris Brown anacheza muziki wa Diamond, ni Bongo Fleva, ni muziki wa kwetu tunajivunia. Hata mimi ningetamani kuona msanii kutoka nje anacheza ngoma yangu, au ya msanii mwingine. Hiki ni kitu kizuri kwetu, hatuko kinyonge nah ii inaonesha tunafanya kazi kweli,” amesema Kiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live