Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kiba: Naweza kufanya Albamu mbili za Amapiano ndani ya wiki (+Video)

Video Archive
Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme kunako game ya Bongo Fleva, Ali Kiba ameweka wazi sababu za kutofanya muziki wa aina ya "Amapiano".

Wengi walitarajia kuona ama kusikia aina hiyo ya muziki katika Albamu ya Ali kiba iliyotoka wiki chache zilizopita inayokwenda kwa jina la "Only one King".

Amapiano ni aina ya muziki ambayo inafanya vizuri hivi sasa Barani Afrika, ikiwemo Tanzania lakini katika Albamu ya mkongwe huyo hakuna ladha ya muziki ya aina hiyo kitu ambacho kimewashangaza wengi.

"Amapiano ni muziki rahisi sana ambao nikisema niufanye naweza kufanya Albamu mbili ndani ya wiki moja"

"Ni muziki mzuri lakini unabebwa sana na beat, kwangu mimi siwezi fanya maana umenipitia kushoto" amesema Kiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live