Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aggy Baby ashinda Tuzo ya ‘100 Most Notable Africans Awards’

Aggy 24 08 12 At 6.jpeg Aggy Baby ashinda Tuzo ya ‘100 Most Notable Africans Awards’

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaharakati wa masuala ya kijamii na Mwanamziki maarufu Tanzania, Agness Suleiman Kahamba amekabidhiwa tuzo yake kupitia taasisi yake ya Tupaze Sauti Foundation baada ya kutangazwa mshindi kipengele cha ‘Notable in community Development’ katika tuzo za ‘100 Most Notable Africans Awards’ zilizofanyika nchini Rwanda.

Hivi ndivyo inavyosadifu kwa mambo anayoyafanya Agness Kahamba, binti wa Kitanzania aliyejipatia umaarufu duniani na kupata tuzo kadhaa kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya muda mfupi katika kutetea haki za wanawake, vijana na watoto.

Tangu mwaka 2018, Agness ambaye ni Mwasisi na Rais wa Tupaze Sauti Foundation (TSF), taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) na Balozi wa Kutetea Unyanyasaji dhidi ya Watoto, ameshatwaa tuzo kadhaa ambazo zimemfanya kuwa miongoni mwa Watanzania waliopata umaarufu katika medani ya kimataifa.

Hivi karibuni, Agness alipata Tuzo ya Wanawake Maarufu Af- rika 2024 (Most Notable Women in Afrika 2024) katika masuala ya familia na maendeleo ya jamii. Tuzo hii imemfanya kuwa mmoja wa watu 100 mashuhuri barani Afrika.

Tuzo hii imekuja baada ya mwaka jana kupata tuzo ya mmoja ya watu 100 wa juu waanzilishi wa NGO. Alipata tuzo hiyo kwa kutetea na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu kwenye masuala ya usawa wa jinsia, ukatili dhidi ya watoto, elimu, afya, uwezeshaji wanawake, haki za binadamu na maendeleo ya jamii.

Tuzo hizo zilikuwa mwendelezo wa ile aliyoipata mwaka 2018 baada ya kushika nafasi ya 16 ya Tuzo ya Vijana 50 wa Tanzania wenye Ushawishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live