Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aburuzwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Mnyeti Pic Mbunge aburuzwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Misungwi Mkoani Mwanza, Alexander Mnyeti amesomewa mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Hata hivyo, Mnyeti hakuwepo mahakamani wakati kesi yake iliposomwa mjini Babati jana Februari 7, 2023 dhidi ya Kampuni ya Uwindaji ya HSK Safaris Ltd ya Wilaya ya Simajiro, kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara kampuni hiyo.

Wakili wake Kuwengwa Ndojekwa ambaye aliiomba mahakama mbele ya Jaji Mfawidhi, John Kahyoza imruhusu aiunganishe serikali kwenye kesi kwa sababu yale anayotuhumiwa kuyatenda yalitendeka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na alikuwa mtumishi wa umma.

Mnyeti anadaiwa kushirikiana na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Emboreet, Belinda Sumari na Salehe Alamry kuinyanganya kitalu cha uwindaji Kampuni ya HSK Safaris Ltd bila kufuata sheria.

Katika shauri hilo namba 2 la mwaka 2022 wadaiwa katika shauri hilo ni Alexander Mnyeti mdaiwa namba moja, mdaiwa namba mbili Belinda Sumari aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Emboreet wilayani Simanjiro na mdaiwa wa tatu Salehe Alamry.

Katika shauri hilo namba 2/2022 la madai Mnyeti anawakilishwa na wakili Kuwengwa Ndejekwa, Salehe Alamry anawakilishwa na wakili Sheki Mfinanga na HSK Safaris Ltd anawakilishwa na Edmond Ngemela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: