Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwijage abariki ujenzi wa kiwanda cha samani za ndani cha Danube na GSM (Video)

Video Archive
Mon, 5 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage amebariki ujenzi wa kiwanda cha samani cha GSM Mall pamoja na kampuni ya kimataifa ya Danube Home.



Kampuni hizo mbili ambazo ninamiliki maduka ya nguo na samani za majumbani nchini Tanzania na Afrika Mashariki, zitajenga kiwanda hicho katika eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari katika makubaliano hayo yaliyofanyika katika duka la Danube Home Mlimani City, Waziri Mwijage amezipongeza kampuni hizo kwa uamuzi wa kukubali ombi lake la kujenga kiwanda ambacho kitatumia malighafi za ndani na wao kutengeneza kuwa bidhaa.

“Tunataka hizi bidhaa ambazo mnaziuza katika maduka yenu kutoka viwanda vyenu vya nje zizalishwe hapa ndani, tunashukuru mmekubali ombi langu na mnafanya hivyo, mimi nawahakikishia wote ambao wana nia ya kutaka kujenga kiwanda nchini wasiwe na wasiwasi, tupo tayari kutatua changamoto zote zitakazo jitokeza,” alisema Waziri Mwijage.

Chanzo: bongo5.com