Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji wa madini waitwa Mara

Madini Manganese Wawekezaji wa madini waitwa Mara

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema wilaya zote ndani ya Mkoa wa Mara zina madini na hivyo anawakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza katika mkoa huo ambao amesema una fursa nyingi.

Kanali Mtambi ameongeza kuwa, mbali na fursa katika sekta ya madini mkoani humo, kuna fursa nyingi pia katika uvuvi, ufugaji, kilimo na utalii.

Kanali Mtambi amesema hayo wakati akiwakaribisha maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambao wapo Kanda ya Ziwa kwenye muendelezo wa kampeni ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live