Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoroshaji wa tumbaku waonywa

Tumbaku Tanzania Watoroshaji wa tumbaku waonywa

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson Ndiege amewaonya baadhi ya Wanaushirika wasio waadilifu wenye tabia ya kutorosha tumbaku na kuuza kwa wanunuzi wasio na mikataba na vyama vyao kuacha tabia hiyo mara moja.

Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanaushirika wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Dkt. Ndiege amesema wanaushirika wachache wanaouza tumbaku kwa wanunuzi wasio na mikataba nje ya utaratibu chama cha ushirika husika wanasababisha changamoto ya vyama kushindwa kulipa madeni ya mikopo benki na hasara kwa mnunuzi mwenye mkataba na chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live