Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii 400 kutoka Hispania wawasili Zanzibar

Watalii Zanzibar Hispania.png Watalii 400 kutoka Hispania wawasili Zanzibar

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zanzibar imepokea watalii 400 kutoka nchini Spain ikiwa ni safari ya kwanza ya moja kwa moja.

Hatua hiyo inatajwa kuongeza idadi ya watalii kisiwani humo.Wamesafiri kwa Shirika la Ndege la World to Fly

Hayo yamesemwa leo Juni 29, 2024 na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Khalid Salum Mohamed alipowapokea watalii hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.

Waziri Khalid amesema huo ni uthibitisho kwamba Zanzibar inazidi kufahamika duniani na hayo ndiyo matunda ya kujitangaza.

"Kwa sasa tuna mashirika 80 ambayo yanaleta ndege zake kisiwani hapa na shirika hili ndiyo mara ya kwanza kuleta watalii moja kwa moja hapa, huu ni wigo mpana katika soko la utalii," amesema.

Amesema ujio wa ndege hiyo utachangia kuongeza pato la Taifa na kuleta ustawi kwa wananchi.

Waziri wa Utalii Zanzibar, Ramadhani Mudrik Soraga amesema hilo ni soko jipya, hivyo watahakikisha wanatanua wigo wa utalii.

Soraga amesema kupitia soko hilo jipya wanatarajia wageni wasiopungua 10,000 watakaofika Zanzibar kwa shughuli za utalii

Chanzo: www.tanzaniaweb.live