Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki wa paka kuanza kulipia leseni

Polisi Waokoa Paka 1,000, Msako Dhidi Ya Biashara Haramu Ya Nyama Ya Paka Wamiliki wa paka kuanza kulipia leseni

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wamiliki wa paka Jijini Nairobi Nchini Kenya hivi karibuni wanaweza kulazimika kupata leseni ili kuendelea kufuga paka kwa ada ya Ksh. 200 (Tsh. 4,131) kwa kila paka wanayemiliki.

Muswada wa sheria ya udhibiti na ustawi wa wanyama katika Kaunti ya Jiji la Nairobi 2024, ambao umewasilishwa katika Bunge la Kaunti ya Jiji hilo unasema hivyo na endapo utapitishwa kuwa sheria Wamiliki wa paka wataanza kulipia leseni hiyo.

Ada hiyo ni kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya utunzaji, udhibiti na ustawi wa wanyama kwa lengo la kukuza uhusiano wa usawa kati ya Wakazi na wanyama.

Muswada huo unasubiri kuidhinishwa na Gavana, Johnson Sakaja na umeratibiwa ukilenga kushirikisha Wananchi mnamo mwezi August 2, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live